Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Papa Leon wa Kumi na nne kupitia mtandao wa kijamii X alijibu ufedhuli wa Trump kwa kusema: Vita, vurugu, dhulma na uongo huumiza moyo wa Mwenyezi Mungu. Moyo wa Baba yetu hauko pamoja na watu waovu, wenye kiburi na majivuno. Moyo wa Mungu uko pamoja na wanyenyekevu na watu wa kujishusha; Yeye pamoja nao hujenga kila siku ufalme wa mapenzi na amani. Popote panapokuwepo mapenzi na huduma, hapo Mwenyezi Mungu yupo.

Maoni yako